Friday, June 7, 2013

KIKAO CHA WADAU WA ULINZI WA MALIASILI MIKOA YA NYANDA YA JUU KUSINI KILICHOANDALIWA NA MRADI WA SPANEST



mkuu wa mkoa  wa Njombe wa pili kushoto Aser Msangi na mkuu wa mkoa wa Iringa Dr Chrstina Ishengoma akiwa na naibu  weaziri  wa maliasili na utalii Lazaro Nyarandu pamoja na mkuu wa mkoa  wa Mbeya Abas Kandoro kulia leo baada ya  kufungua  semina  hiyo 




HOTUBA YA MHESHIMIWA LAZARO NYALANDU NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII, KWENYE MKUTANO WA WADAU WA MTANDAO WA KUBORESHA ULINZI WA MAENEO YA HIFADHI KUSINI MWA TANZANIA (SPANEST) UTAKAOFANYIKA KATIKA UKUMBI WA VETA, IRINGA, TAREHE 4 NA-5 JUNI 2013


·        Mheshimiwa Dr. Christine Ishengoma - Mkuu wa Mkoa wa Iringa;
·        Waheshimiwa Wakuu wa Mikoa ya Njombe, Mbeya na Dodoma;
·        Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii
·        Mkurugenzi wa  Idara ya Wanyamapori;
·        Wakurugenzi Wakuu wa TANAPA na TAWIRI;
·        Wageni waalikwa;
·        Mabibi na Mabwana; (Itifaki imezingatiwa)
·        Awali ya yote, nichukue fursa hii kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutusafirisha salama hadi mahali hapa na kutupa uzima na afya njema kwa ajili ya mkutano huu muhimu. Kwa dhati kabisa ninaushukuru uongozi wa Mradi wa Kuboresha Mtandao wa Maeneo ya Hifadhi Kusini mwa Tanzania (SPANEST) kwa kunialika na kunipa heshima ya kuwa Mgeni Rasmi katika kufungua mkutano huu.
Nimearifiwa kuwa huu ni mkutano wa wadau ambao watakuwepo hapa kwa siku mbili kujadili kwa kina ulinzi wa maliasili hususan wimbi la ujangili wa tembo kwenye maeneo ya hifadhi na mapori ya akiba katika Mikoa ya Nyanda za Juu Kusini. Ninatambua kuwa uwepo wenu na kupitia fursa ya mkutano huu mtatoa michango yenu muhimu katika kufanikisha jitihada za Wizara yangu na Serikali kwa ujumla katika kukabiliana na wimbi la ujangili wa tembo ndani na nje ya maeneo yaliyohifadhiwa.
Mabibi na Mabwana,
Nchi yetu imebarikiwa kuwa na rasilimali nyingi za maliasili hususan wanyamapori ambao ni kivutio kikubwa cha utalii – utalii unaoegemea wanyamapori (wildlife-based tourism). Aidha, watalii wengi wanaotembelea hifadhi na mapori yetu ya akiba huvutiwa sana na tembo ambaye pia ni mnyama mwenye mchango mkubwa kiikolojia (keystone species).  Ukanda wa Kusini mwa Tanzania wenye Hifadhi za Taifa za Ruaha na Katavi, Mapori ya Akiba Rungwa, Muhesi na Kizigo ni miongoni mwa maeneo ambayo bado yana idadi kubwa ya Tembo. Idadi hiyo inafikia takriban tembo 30,000 kwa sasa.
Mabibi na Mabwana,
Tafiti zinaonyesha kuwa ujangili na uharibifu wa mazingira kwa pamoja vimechangia kupungua kwa idadi ya tembo duniani, ambapo takwimu zinaonesha kuwepo tembo  milioni 50 mwaka 1930  na sasa wamepungua na kubakia tembo 402,067 tu (Hii ni kwa mujibu wa CITES).

Tanzania pia, ambayo ni nchi ya pili barani Afrika kwa kuwa na idadi kubwa ya tembo baada ya Botswana yenye tembo 154,658, imeendelea kupoteza tembo wake. Idadi ilipungua kutoka kati ya 250,000 na 300,000 katika miaka ya sitini (1960s) hadi 55,000 miaka ya themanini (1980s). Baada ya Serikali kuchukua hatua mbalimbali kudhibiti ujangili, ikiwemo “OPERESHENI UHAI”, idadi iliongezeka na kufikia 141,000 mwaka 2006. Lakini, ilipofika mwaka 2009 idadi ilikuwa imepungua tena na kubakia tembo 110,000 tu (Hii ni kwa mujibu waTAWIRI).
Kupungua huku kunatokana na ujangili, ambao ulisababishwa na mambo kadhaa yakiwemo mahitaji makubwa ya meno ya tembo katika soko haramu kwenye nchi za Mashariki ya Kati na Mbali, faida kubwa inayotokana na biashara ya meno ya tembo, umasikini wa wananchi wetu, rushwa na mmomonyoko wa maadili kwa watumishi wa umma. Masuala mengine yanayoweza kuwa yamechangia katika kupungua kwa idadi ya tembo ni pamoja na mabadiliko ya tabianchi, majanga ya asili na magonjwa.
Ujangili huu si tu unahatarisha kupotea kwa tembo na baadhi ya spishi za wanyamapori zinazotegemea ecosystems walimo tembo, bali pia unaathiri utalii kwa ujumla wake. Aidha, hali hii inaashiria kutokuwepo amani na usalama si tu wa hifadhi zetu bali pia wa wananchi na uchumi wa nchi kwa ujumla. Hili linaweza kuwa geni katika masikio ya baadhi yetu. Nikirejea kwenye utalii, ujangili unathiri kwa kiasi kikubwa idadi ya watalii wanaotutembelea na, kama matokeo yake, kuathiri pato la taifa – ambalo linategemea utalii kwa asilimia 17.
Mabibi na Mabwana,
Ili kukabiliana na mtandao mkubwa wa ujangili wa kimataifa unaotumiatekinolojia na silaha za kisasa, ni budi kujizatiti kwa kuongeza uwezo wa kukabiliana na njama hizi zinazotishia kupotea kwa tembo katika uso wa dunia katika karne hii. Ninaamini mkutano huu utajadili kwa kina na kubainisha changamoto zilizopo na majadiliano mtakayoendesha yatalenga kuzipatia ufumbuzi changamoto zinazoikabili sekta ya ulinzi wa rasilimali za wanyamapori hususan tembo dhidi ya ujangili na uharibifu wa mazingira kwa ujumla wake. Ni matarajio yangu kwamba kikao hiki kitatoa dira ya kuboresha uhifadhi katika zama hizi ambazo majangili wanatumia mbinu za kisasa kutekeleza azma yao chafu.

Mabibi na Mabwana,
Nimalizie kwa kuwashukuru waandaji wa mkutano huu (SPANEST) na kuwatakia washiriki mkutano wenye mafanikio makubwa. Ni imani yangu kuwa mchango wa kila mshiriki utatoa mwelekeo wa kulitokomeza kabisa tatizo la ujangili nchini mwetu. Aidha, Ni matarajio yangu kwamba maazimio ya mkutano huu yatakuwa chachu ya kuboresha uhifadhi katika kanda ya kusini na Tanzania kwa ujumla.


ASANTENI SANA KWA KUNISIKILIZA

Sunday, May 12, 2013

IRINGA REGIONAL TOURISM MEETING

     The SPANEST project was pleased to be able to organise a regional tourism meeting in Iringa on 5-6 march 2013. 

     The Assistant Director of Tourism from MNRT, TANAPA ,TTB team and TTB Cultural Tourism Program Coordinator from Arusha, plus district level officials from all Iringa districts, a representative from Mbeya region and the private sector attended the meeting which was chaired by Iringa RC.


                                                        Dr Ezekiel Dembe, TANAPA


MNRT, TANAPA & TTB Southern Circuit Office Representatives  




Godwell Old Meing'ataki - SPANEST PC