STORIES

WANAOZUNGUKA HIFADHI ZA TAIFA WATAKIWA KUWA NA MIPANGO BORA YA MATUMIZI YA ARDHI

ILI kunusuru rasilimali zinazoendelea kupotea katika hifadhi za Taifa, halmashauri za wilaya zinazozunguka maeneo hayo zimetakiwa kuwa na mipango bora ya matumizi ya ardhi.
Katika kuhakikisha lengo hilo linafikiwa, mradi wa Kuboresha Mtandao wa Maeneo ya Hifadhi Kusini mwa Tanzania (SPANEST) umeanza kutoa mafunzo hayo kwa watendaji wa halmashauri zinazozunguka hifadhi za kusini.
Mratibu wa SPANEST, Godwell Meing’ataki alisema mafunzo hayo ya siku tano yanahusisha watendaji kutoka halmashauri za wilaya ya Mbeya, Wanging’ombe, Makete, Chamwino, Katavi na Iringa.
“Na wawakilishi kutoka hifadhi ya Ruaha, Mikumi, Udzungwa na Kitulo; na mapori ya kiba ya Rungwe, Mpanga Kipengele na Rungwa, Mhesi na Kizigo,” alisema.
Meing’ataki alisema halmashauri zinazozunguka hifadhi za Taifa zinatakiwa kuwa na mipango bora ya matumizi ya ardhi ili kuepukana na migogoro inayopelekea baadhi ya wananchi wake kuvamia kwa matumizi yao maeneo mbalimbali yaliyohifadhiwa.
“SPANEST tunaamini tunachofanyakifanya kwenu kwa siku hizi tano hakitakuwa na umuhimu kama hakitaleta matokeo yoyote chanya baada ya kumaliza mafunzo haya,” alisema.
Akifungua mafunzo hayo jana, Katibu Tawala Msaidizi wa Mkoa wa Iringa, Adam Swai alisema ardhi ni rasilimali ya msingi; ili kukidhi mahitaji yake hapana budi watumiaji wake wae na utaratibu na mipango itakayoathiri wengine.
Mwakilishi kutoka Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi, Jarome Nchimbi ambaye ni mkufunzi wa mafunzo hayo alisema sheria ya mipango ya Matumizi ya Ardhi Namba 6 ya mwaka 2007 imeweka misingi ya kupanga matumizi hayo ya ardhi.
Alisema Mpango wa Matumizi Bora ya Ardhi ni utaratibu wa kutathimini na kupendekeza namna mbalimbali za uhifadhi na matumizi ya maliasili au rasilimali ili kuinua uchumi wa Taifa na kuondoa umasikini.
Alisema katika mafunzo hayo, washiriki watajidiliana tishio dhidi ya viumbe hai vilivyohifadhiwa na matumizi bora ya ardhi kama njia muafaka ya kukabiliana na migogoro ya ardhi.
Mengine ni sera na sheria zinazosimamia matumizi bora ya ardhi, mipango ya kina ya usimamizi wa ardhi, mbinu za usuluhishi wa uatatuzi wa migogoro ya mipaka, tathmini shirikishi ya matumizi ya ardhi na mipaka na hali halisi ya matumizi ya ardhi ya kijiji.

UNDP YAIPIGA JEKI HIFADHI YA RUAHA NA KITULO, NI MAGARI MATATU NA GREDA MOJA



SHIRIKA la Hifadhi za Taifa (TANAPA) limepokea msaada wa vitendea kazi vitakavyosaidia kuimarisha ulinzi na miundombinu ya barabara kutoka Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP).

Msaada huo uliotolewa kupitia Mradi wa Kuimarisha Mtandao wa Maeneo ya Hifadhi Kusini mwa Tanzania (SPANEST) unahusisha magari matatu aina ya Toyota Pickup na greda moja.

Hati za makabidhiano zilisainiwa jana huku upande wa UNDP ukiwakilishwa na Naibu Mkurugenzi Mkaazi wa UNDP hapa nchini, Mandisa Mashologu na TANAPA ikiwakilishwa na Kaimu Mkurugenzu Mkuu wake, Dk Ezekiel Demba.

Kwa kupitia msaada huo, Mratibu wa SPANEST, Godwel Ole Meing’ataki alisema hifadhi ya Taifa ya Ruaha imepata greda na magari mawili huku Hifadhi ya Kitulo ikiondoka na gari moja.

Naibu Mkurugenzi Mkazi wa UNDP, Mashologu alisema msaada wa magari utasaidia kupunguza changamoto inayowakabilia askari wanyamapori katika kukabiliana na vitendo vya ujangili huku greda hilo likitumika kuimarisha miundombinu ya barabara katika hifadhi na vijiji jirani.

“Juzi nilipata fursa ya kutembelea hifadhi mara baada ya kufika hapa Ruaha, nachoweza kusema ni kwamba kukiwa na mtandao mzuri wa barabara utahamasisha watalii wengi kutembelea hifadhi hiyo,” alisema.

Kwa upande wake, Dk Dembe alisema “UNDP wametambua umuhimu wa hifadhi zetu za Taifa tunazohifadhi sio kwa manufaa ya taifa tu bali dunia nzima.”

Alisema tofauti na watu wengi wanaodhani TANAPA kuna fedha zinazotiririka kama maji, ukweli ni kwamba haina uwezo wa kufanya uhifadhi bila msaada wa wadau wengine wakiwemo UNDP.

Mkurugenzi wa Uhifadhi TANAPA, Martin Loiboki alisema katika hafla hiyo kwamba vitenda kazi hivyo vitakuwa na mchango mkubwa kwa TANAPA na maeneo jirani na hifadhi.

Alisema hifadhi ya Ruaha ndiyo hifadhi yenye tembo wengi kuliko maeneo mengine yoyote yaliyohifadhiwa hapa nchini.

“Tembo ni mnyama aliye katika hatari kubwa kuliko mnyame mwingine; msaada huu ni muhimu sana kwa hifadhi ya Ruaha kwasababu kabla ya kuupokea ilikuwa na magari sita tu ya doria,” alisema.

Katika kukabiliana zaidi na ujangili Mratibu wa SPANEST alisema mifumo ya mawasiliano ya kisasa itafungwa katika magari hayo na vituo ili kuwezesha kazi ya kukabiliana na majangili kufanyika kwa ukamilifu.



WATOA HUDUMA MBALIMBALI WAKIWEMO WA SERIKALI NA TAASISI BINAFSI KAMA MAHOTELI MAKAMPUNI NA BIASHARA MBALIMBALI WANOLEWA LEO MKOANI NJOMBE



Mkuu wa mkoa wa Njombe Captain mstaafu Aseri Msangi  amefungua mafunzo ya siku mbili

kwa watumishi mbalimbali wa serikali na taasisi binafsi mkoani Njombe ambapo pamoja  na

mambo mengine amewataka watumishi hao kutumia fursa hiyo katika kufikia malengo

yaliokusudiwa ili kuibadilisha jamii ya mkoa wa Njombe.

Akizungumza na watumishi mbalimbali katika ufunguzi wa semina ya watoa Huduma Mkuu wa

mkoa wa Njombe Msangi amesema kuwa licha yakuwa tumepewa mkoa bado wafanyabiashara na

watoa huduma mbalimbali hawajaanza kuweka mahitaji kwa kiwango kinachostahili ambapo

amesema ili kubadilisha mkoa uwe na sifa nzuri watoa huduma wanatakiwa kuboresha huduma

zao.

Aidha Msangi amesema kuwa mkoa wa Njombe ni miongoni mwa mikoa yenye vivutio vingi vya

kiutalii na kwamba watoa huduma mbalimbali wa serikali na taasisi binafsi wasipojipanga

kikamilifu watashindwa kutoa huduma nzuri kwa wateja ambapo ametolea mfano hotel zilizopo

mkoani hapa kwamba bado hazijafikia madaraja yanayotakiwa na yakuwavutia watalii mbalimbali

mkoani hapa.

Amesema kuwa watoaji wa huduma wanatakiwa kuwa na muonekano mzuri kwa wateja wake

huku akiwataka kuwa na Elimu,ujuzi na maarifa pamoja na kuzingatia matumizi ya kauli zao kwa

mkila eneo na kwamba mafunzo hayo yataleta mabadiliko kwa watoa huduma mbalimbali mkoani

Njombe.

Akizungumza mara baada ya kufunguliwa kwa semina hiyo mratibu wa mradi wa kuboresha

mtandao wa maeneo yaliohifadhiwa kusini mwa Tanzania bwana Godwell Ole Meing'ataki

amefafanua maana ya utalii na kwamba utalii ni sekta  pana ambayo inatazama maeneo

mbalimbali ikiwemo ya utoaji wa huduma kwa jamii ambayo inahitaji umakini na uelewa mkubwa

ili kuwavutia watalii.

Aidha bwana Meing'ataki amesema kuwa awatoaji wa huduma kwa jamii wanatakiwa kuzingatia

mambo mbalimbali ikiwemo kufungua njia za usafiri kama barabara,nyumba za kulala

wageni,kuboresha huduma za chakula,mawasiliano mazuri, viwanja vya ndege na kwamba mtoaji

huduma anatakiwa kumuelewa mteja wake ili siku nyingine aweze kurudi tena badala ya

kukasilishwa na huduma na kushindwa kurudi tena.

Ernest Mkongo ni mwenyekiti wa Utalii mkoa wa Njombe amesema kuwa wahusika wa mafunzo

hayo ni pamoja na watumishi wa halmashauri,taasisi binafsi ikiwemo hotel,madereva wa magari,

na sekta mbalimbali ambazo zinatoa huduma kwa jamii za kiofisi na zisizo za kiofisi ambapo

pamoja na mambo mengine amesema washiriki wa mafunzo nhayo wameweza kutokea

halmashauri ya mji wa Njombe,wilaya ya Njombe na halmashauri ya mji wa Makambako

nakwamba awamu nyingine yatakwenda kwa watumishi wa halmashauri zilizobaki za

Wanging'ombe,Makete na Ludewa.

Mafunzo hayo yalioandaliwa na shirika la SPANEST  yaani kirefu chake ni Streghening The

Projected  Network in Southern Tanzania yamelenga kuleta mabadiliko kwa watoa huduma

mbalimbali nyanda za juu kusini mwa Tanzania ambapo huo ni mradi wa pamoja kati ya shirika la

maendeleo la Umoja wa mataifa UNDP kwa kushirikiana na shirika la hifadhi la Taifa Tanzania

TANAPA.

 Mradi huo umekuwa ukitekelezwa yapata mwaka wa pili sasa ambao ni mradi wa miaka mitano

katika mikoa ya Nyanda za juu kusini ya Iringa,Mbeya na Njombe ambao umekuwa ukilenga

kuhamasisha uboreshaji wa utoaji wa huduma na kuleta ushirikiano kwa wadau mbalimbali kwa

kusimamia hifadhi zilizopo na kukabiliana na changamoto zinazoweza kuleta athali katika maeneo

ya hifadhi na kwamba changamoto kubwa ni katika mbuga ya hifadhi ya Ruaha ya Ujangiri na

kukauka kwa mto Ruaha. 




No comments:

Post a Comment